- Ni swali la tangu jadi kuhusu umri unaostahili kwa mtu kushiriki ngono kwa mara ya kwanza
- Waumini wa kidini wanasema wakati huo spesheli unastahili kuwa katika ndoa, lakini wanasayansi wa Uingereza wanatofautiana na msimamo huo tena vikali sana
13! Huo ndio umri tosha wa kuanza ngono, utafiti wasema
Watafiti katika Chuo Kikuu cha Cambridge nchini Uingereza yaonekana wamepata jibu la mjadala mkali wa tangu jadi ambalo umewafanya wengi kujikuna vichwa bila mafanikio; hususan matineja na wazazi ama walezi wao: je, umri upi sawa wa kuanza kushiriki ngono?
Kwa mujibu wa wanasayansi hao, umri wa kadri ambao mtu anastahili kushiriki ngono kwa mara ya kwanza ni miaka 13, kutoka 18 miaka ya 1880.
Habari Nyingine: Wapenzi wacharazwa kwa kushiriki ngono kichakani
Mmoja wa watafiti hao Ken Ong aliambia shirika la habari la AFP kuwa maisha ya anasa katika karne ya sasa imechangia pakubwa kupunguza umri huo, kigezo kikuu ni maumbile ya mtu:jeni za DNA.
Ni DNA ya mtu inayochangia pakubwa masuala kama kubaleghe kwa tineja. Wanasayansi hao wa Cambridge walichunguza DNA za watu 380,000 na kubaini kuwa jeni zao ndizo zinachangia pakubwa uamuzi wa mtu kuvunja ubikra.
Habari Nyingine: Mwanamke matatani kwa kutafuta ngono kwa Facebook
Utafiti huo ulisaidia kubaini mchango wa vigezo vingine vinavyomsukuma mtu kuanza ngono ama kujifunga kamba hadi utu uzima: uthabiti wa familia na ushawishi wa marafiki wa rika moja.
Vile vile, wanasayansi wametaja mabadiliko ya lishe, unene wa watoto wa siku hizi na kemikali zinazothiri homoni za mwili.
Matokeo ya utafiti huo yanakujia wakati ambapo maafisa wa usimamizi Kenya wanazidi kudhibiti aina ya vipindi na matangazo yanayopeperushwa katika vyombo vya habari, ambayo yanaweza kuwatia nyege zisizostahili vijana wachanga.
Habari Nyingine: Mawazo 10 ya wanawake kabla ya kujihusisha kwa ngono
Bodi ya Kudhibiti Filamu Kenya imetayarisha kanuni mpya kuhusu matangazo ambayo yanatumia watu wakiwa uchi ama nusu uchi, kondomu zilizopigwa marufuku na matangazo mengine yanayoashiria ngono kwa sana.
Suala la ngono nchini Kenya, kama ilivyo katika jamii nyingi za Afrika, ni mada inayojadiliwa kwa minong'ono.
Read ENGLISH VERSION