Abura Achieng aliaga akipokea matibabu katika hospitali kuu ya Kenyatta, jana Alhamisi, tarehe 20, wakati wakenya wakisherehekea siku kuu ya Mshuajaa. Yeye ni shujaa pia!
Kifo chake kimeuzunisha wakenya wengi huku wengi wakionyesha masikitiko yao katika kurasa zao za facebook na twitter.
Alikuwa ameandika jumbe kwa mtandao kuhusu hali yake ya afya.
Habari Nyingine: Nimelala na wanaume elfu tano kwa miaka ishirini, asema Kahaba
" Kwa muda wa miaka mitatu, nimepoteza kilo hamsini. Najihisi mlegevu na mnyonge na daktari ananiambia niongeze kilo thelathini. Cha kushangaza ni kuwa sikutaka mwenyewe nipungue, bali hali ya mwili wangu ilizidi kudorora. Pateni somo kutoka kwa makosa yangu!" Vile aliandika kwa ukurasa wake wa Facebook.
Abura, mama wa mtoto mmoja alikiwa mwimbaji wa Afro-Jazz na nyimbo za injili. Alikuwa pia mtunzi wa nyimbo na mcheza kinanda
Habari Nyingine: Mambo matano usiyoyajua kumhusu Raila Odinga
Achieng kwa wakati mmoja alikuwa mkufunzi wa wanamuziki wa Tusker Project Fame.
Alikuwa mfano wa kuigwa kwa wakenya wengi hasa kwa wanamuziki wachanga.
Sauti yake tamu itabakia kukumbukwa na wengi na atabaki katika nyoyo ya watu wengi.
Achieng Abura, Pumzika kwa amani
PICHA: Hisani
Read the ENGLISH VERSION