Staa wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake wa Nitasubiri, Juma Khalid ‘Jux’.
MALOVEE! Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, staa wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake wa Nitasubiri, Juma Khalid ‘Jux’, kwa mara ya kwanza amevunja ukimya na kufungukia penzi lake na modo anayedaiwa kufungwa nchini China kwa msala wa madawa ya kulevya ‘unga’, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’.
Jux ambaye anasoma nchini China huku akifanya muziki wa Bongo Fleva, alifunguka hayo juzikati katika ‘exclusive interview’ aliyoifanya na mwanahabari wetu alipokuwa mjini Kahama alipokwenda kwenye Serengeti Fiesta 2014.
Akijibu swali la mwandishi wetu lililomtaka afungukie penzi lake na Jack ambalo alikuwa akichengachenga kila alipotakiwa kutoa ufafanuzi na vyombo vya habari, Jux alianza kwa kukiri kwamba mrembo huyo alikuwa mpenzi wake na walidumu kwa takriban miezi saba kabla hajakutwa na msala wa madawa ya kulevya.
Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’.
Alisema tangu aanze kuyajua mapenzi, Jack alikuwa ni mwanamke wa pekee kwake ingawa wakati anapatwa matatizo walikuwa wametibuana kwa kipindi cha wiki mbili.
“Nilisikitika sana niliposikia amekamatwa kwa madawa ya kulevya, nilikuwa sijui kama anafanya hiyo biashara na kinachoniumiza zaidi ni kwamba nilikuwa najua yupo Bongo na nikajua tutaonana maana mimi nilikuwa Bongo wakati huo,” alisema Jux.XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Alipoulizwa kama ana taarifa za Jack kufungwa miaka sita jela kama ilivyoripotiwa wiki iliyopita, Jux alisema hana taarifa hizo.“Kiukweli sijazipata habari hizo labda nitakapoenda tena China ndiyo nitajua kupitia kwa mwanasheria wake maana kwa sasa hajanipa taarifa na hana namba yangu ya simu ya hapa,” alisema Jux.
Jux akiwa na Jack Patrick.
Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka jana akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong Kusini mwa China.