2014-03-19



 Kaimu mkurugenzi wa  biashara na masoko wa shirika la ndege la Air Tanzania, Juma Boma (wa pili kulia) akipanda ndege mpya aina ya CRJ-200 katika uwanja wa ndege Julius Nyerere muda mfupi kabla ya kuondoka kwenda uwanja wa ndege wakimataifa wa Songwe. Shirika hilo limeanza safari zake kwenda Mbeya ambapo itaruka mara nne kwa wiki.



 Kaimu mkurugenzi wa biashara na masoko wa shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) Juma Boma akipokea maua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa ndege hiyo, muda mfupi baada ya kushuka kwenye ndege yao mpya aina ya CRJ-200 iliyotumika  kuzindua safari za kati ya Dar es Salaam na Songwe. Nyuma yake ni kaimu mkurugenzi wa ufundi, Patrick Itule. Shirika hilo litakuwa linaruka mara nne kwa wiki kwenda Mbeya. 



 Kaimu mkurugenzi wa  biashara na masoko wa shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) Juma Boma, akibadilishana mawazo na Kaimu mkurugenzi wa ufundi wa shirika hilo, Patrick Itule, muda mfupi baada ya kushuka kwenye ndege yao mpya aina ya CRJ-200 inayotumika katika uzinduzi wa safiri kati ya Dar es S alaam na Mbeya. Shirika hilo litakuwa likifanya safari zake mara nne kwa wiki kwenda Mbeya, safari ya lisaa limoja tu.

 Meneja wa Kanda ya Mbeya wa shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL), Shabani Mtambalike (kulia), akimkaribisha Kaimu mkurugenzi wa biashara na masoko wa ATCL, Juma Boma (wa pili kulia) na kaimu mkurugenzi wa ufundi Patrick Itule muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Songwe Jumatatu mchana. Shirika hilo lilitumia ndege yake mpya aina ya CRJ-200 kuzindua safari zake ambapo itasafiri mara nne kwa wiki.

 Kaimu mkurugenzi wa  biashara na masoko wa shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) Juma Boma (wa pili kulia, Kaimu mkurugenzi wa ufundi Patrick Itule (wa tatu kulia) na Meneja wa Kanda ya Mbeya wa shirika hilo Shabani Mtambalike (kulia) wakishangilia, pamoja na wageni wengine, kuwasili kwa ndege ya ATC katika uwanja wa ndege wakimataifa wa Songwe  jumatatu mchana. Shirika hilo lilitumia ndege yake mpya aina ya CRJ-200 kuzindua safari zake ambapo itasafiri mara nne kwa wiki.

 Kaimu mkurugenzi wa  biashara na masoko wa shirika la ndege la Air Tanzania Juma Boma akikata keki kama ishara ya kuzindua safari za ndege ya ATCL kati ya Dar Es Salaam na Mbeya, hafla iliyofanyika katika uwanja wa ndege wa Songwe siku ya Jumatatu mchana. Shirika hilo la ndege lilitumia ndegeyake mpya aina ya CRJ-200 kuzindua safari zake ambapo itasafiri mara nne kwa wiki

 Abiria wakiwa ndani ya ndege mpya ya Air Tanzania aina ya CRJ-200 muda mfipi kabla ya kutua katika uwanja wa ndege wa  Songwe wakitokea Dar es Salaam. 

Abiria wakipanda ndege ya Shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) aina ya CRJ-200 katika uwanja wa ndege wakimataifa wa Songwe wakielekea Dar es Salaa. Safari hizi zitafanyika mara nne ndani ya wiki.

========  ========    =========

ATCL yaanza safari za kwenda Mbeya  

Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) Jumatatu hii lilizindua safari zake za kwenda Mbeya kupitia uwanja mpya wa ndege wa kimataifa wa Songwe likitumia ndege yake mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 50 ya Canada aina ya CRJ – 200.

Safari hiyo inayochukua kadri ya saa moja kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya itakayofanyika siku nne kwa wiki; Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili, ililakiwa na abiria na wafanyabiashara wanaosafiria kutoka Mbeya kwenda katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam.

Akizungumza katika uzinduzi wa kihistoria uliofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe, Kaimu Mkurugenzi wa Biashara/Masoko wa shirika hilo Bw. Juma Boma alisema Air Tanzania imerudi kwa kishindo katika mji ambao ni kitovu cha biashara kwa mikoa ya nyanda za juu kusini na inayotumika kama njia ya kuiunganisha Tanzania na nchi za Kusini mwa  Afrika, ili kupunguza adha ya usafirina kuiunganisha sehemu ya Kusini mwa Tanzania na mikoa mingine.

“Safari ya Air Tanzania kwenda Mbeya iliyosubiriwa kwa muda mrefu imeanza rasmi leo hii. Kwa kutumia ndege yetu mpya, tunatoa usafiri wa haraka na salama, tukiiunganisha Mbeya na mikoa mingine. Kwa saa moja tu, abiria wetu wanauhakika wa kutua uwanja wa ndege wa Songwe kutokea Dar es Salaam.

“Tumezingatia masuala yote ya kiuchumi ili kupanga nauli tuliyoanza nayo ambayo ni kiasi cha shilingi 150,000 kwa tiketi ya kwenda na shilingi 260,000 kwa tiketi ya kwenda na kurudi,” alisema,” Bw. Boma.

Alisema uzinduzi wa njia ya Mbeya ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati madhubuti wa upanuzi wa shirika, ambao umelenga katika kuzirejesha safari zote za ndani na za kimataifa na kufungua njia nyingine mpya.

Boma alisema kuwa kutokana na mkakati wao ujulikanao kama go-green utalipelekea shirika hilo la ndege la taifa kuongeza toleo jipya ya ndege nyingine mbili zenye uwezo wa kubeba abiria 78 mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu, shirika hilo litaongeza idadi ya safari zake katika njia zake kuu na kuongeza safari za kimataifa.

“Kupitia upanuzi wa safari zetu, abiria wetu watafurahia safari za kila siku kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, ikiwa muda wa kuondokea Dar ukiwa ni saa 11 jioni na kutokea Mwanza  ni saa moja usiku. Tutakuwa tukienda mwanza mara nne kwa wiki.

 Tutakuwa pia tukisafiri kwenda Moroni nchini Comoro katika siku za Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumamosi. Vile vile tunatarajia kufungua njia ya Tabora – Mpanda hivi karibuni,” alisema.

Alibainisha kuwa shirika hilo pia limeondoa baadhi ya adhabu watozwazo abiria wanaoshindwa kutokea wakati wa safari na wale wanaobadilisha ratiba ya safari zao, na kusema kuwa hii itawasaidia abiria wao kutoingia gharama za ziada endapo watakumbana na dharura mbali mbali kabla ya safari.

Mmoja kati ya abiria aliyesafiria katika ndege hiyo kwenda Mbeya, Deogratius Nyanshile aliipongeza Air Tanzania kwa maamuzi yake na kutoa wito kwa watanzania kuliunga mkono shirika kwa kusafiria na Air Tanzania.

“Nawaasa wakazi wa mkoa wa Mbeya na kanda ya kusini kwa ujumla, kuitumia fursa hii kikamilifu iliyotolewa na shirika la Ndege la Air Tanzania,” alisema Nyanshile. Ndege hiyo ya taifa, ambayo ilisimamisha huduma zake katika mkoa huo kwa sababu ya ubovu wa uwanja wa ndege wa zamani wa Mbeya, imerejesha safari hizo baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe.

Ikitumia ndege yake aina ya  Bombardier Dash-8, ATCL kwa sasa shirika hilo linasafiri katika zaidi ya sehemu naneTanzania ikiwa ni pamoja na Mtwara, Mwanza,  Tabora,Kigoma, Dar es Salaam, Bujumbura, Mbeya na kwendaMoroni nchini Comoro.

Show more